Klabu ya Manchester United inaweza kupindua meza mbele ya Real Madrid kwa kumsajili kinda wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri (18) Leny Yoro anayekipiga ndani ya klabu ya Lille.
Kinda Leny Yoro ambaye amekua kwenye ubora ndani ya kikosi cha Lille amekua akifukuziwa na klabu ya Manchester United katika dirisha hili, Lakini klabu ya Real Madrid ndio imeonekana kua na nguvu zaidi kwa beki huyo kwani mabingwa hao wa ulaya wanapewa nafasi kubwa na mchezaji mwenyewe.Man United walipeleka ofa ya Euro milioni kwa 50 kwa klabu ya Lille na ikakubaliwa lakini changamoto ikiwa kwa mchezaji huyo ambaye anataka kukipiga ndani ya Real Madrid, Lakini uongozi wa klabu ya Lille unapambana kuhakikisha mchezaji huyo anajiunga na Man United.