Mbappe kama Ronaldo tu

Nyota wa zamani wa klabu ya PSG Kylian Mbappe amefanikiwa kutambulishwa ndani ya klabu ya Real Madrid baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu hatimae leo jambo hilo limetimia.

Kylian Mbappe amefanikiwa kutambulishwa katika dimba la Santiago Bernabeu kwa ukubwa uleule ambao staa ambaye ni kioo kwa nyota huyo Cristiano Ronaldo alitambulishwa nao ndani hilo mwaka 2009, Huku yeye miaka 14 mbeleni akija kufata nyendo za mchezaji ambaye kwake ni kioo.mbappeStaa huyo ametambulishwa leo katika dimba la Bernabeu ambapo mashabiki zaidi ya elfu 80 wamehudhuria katika utambulisho huo, Hii ikienda sambamba na Cristiano Ronaldo ambaye alitambulishwa pia kwa idadi hiyo kubwa ya mashabiki kuhudhuria uwanjani na wote hao wakiwa wanashikilia rekodi ya kuingiza mashabiki wengi kwenye utambulisho wao.

Halikadhalika staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa wakati wa utambulisho wake alionekana kufanya vitendo kadhaa ambavyo alivifanya pia Cristiano Ronaldo wakati anatambulishwa mwaka 2009, Hata alipoulizwa alikubali na kusema ni heshima ameitoa kwa mtu ambaye amemvutia zaidi kwenye mpira.mbappeBaada ya utambulisho wa Mbappe kukamilika leo na kuonekana kufanana kwa kiasi kikubwa na ule wa Cristiano Ronaldo mwaka 2009 ambaye ni mchezaji pendwa wa staa huyo wa zamani wa PSG, Jambo kubwa lililobaki ni Mbappe kuweza kufanya makubwa ndani ya Real Madrid kama alivyofanya Ronaldo ili kuiweka historia inayofanana zaidi.

Acha ujumbe