Mbappe Kutambulishwa Jumanne ijayo Bernabeu

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ambaye kwasasa ni mchezaji wa klabu ya Real Madrid Kylian Mbappe kutambulishwa Jumanne ya tarehe 16 mwezi pale Santiago Bernabeu.

Mbappe atatambulishwa katika dimba la Santiago Bernabeu kama magwiji waliopita klabuni hapo  walivyotambulishwa, Siku ya Jumanne itakua ni siku ya sikukuu kwa mashabki wa Real Madrid kwani wataenda kumuona mchezaji wao waliomsubiri kwa takribani miaka minne.mbappeStaa huyo wa kimataifa wa Ufaransa anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia klabu ya Real Madrid kwa maana atakua klabuni hapo mpaka mwaka 2029, Lakini pia mabingwa hao wa ulaya watakua na uwezo wa kuendelea kua nae zaidi kama watahitaji kumuongezea mkataba.

Kinachosubiriwa kwa hamu zaidi ni kuona kama mshambuliaji Kylian Mbappe ataweza kuvunja rekodi ya Cristiano Ronaldo, Ambaye aliweka rekodi ya utambulisho wake kuhudhuriwa na watu wengi zaidi sasa Jumanne ndio inaweza kua siku ya rekodi kuvunjwa au ikaendelea kubaki hai.mbappeMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Real Madrid kuelekea msimu ujao akishirikiana na raia wa wawili wa kimataifa wa Brazil Vinicius Jr pamoja na Rodrygo Goes, Huku kitendawili kikiendelea kubaki kati yake na Vinicius Jr nani atacheza upande wa kushoto.

Acha ujumbe