Manchester United Hatimae Yakamilisha Dili Lake la Kwanza

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kukamilisha dili lake la kwanza katika majira haya ya joto baada ya kumsajili aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Bologna Joshua Zirkzee.

Manchester United imekamilisha dili la Joshua Zirkzee leo baada ya mazungumzo ya takribani mwezi mmoja baina ya vilabu hivo, Mchezaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano ndani ya Man United huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.manchester unitedMashetani wekundu wamekataa kulipa kiasi cha €40 milioni ambacho kilikua kimewekwa kwenye mkataba wa mchezaji huyo kwa klabu yeyote itakayomuhitaji itapaswa kulipa kiasi hicho, Badala yake wamekubali kulipa kiasi cha €42 milioni kidogo kidogo kwa muda wa miaka mitatu.

Joshua Zirkzee anajiunga na Man United baada ya kufanya vizuri ndani ya klabu ya Bologna msimu uliomalizika na kua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha kocha Thiago Motta, Mashetani wekundu wanatarajiwa kua na washambuliaji wawili sasa wenye umri mdogo kwenye kikosi chao lakini wenye aina tofauti ya uchezaji Zirkzee pamoja na Hojlund.manchester unitedMshambuliaji Joshua Zirkzee atasafiri kuelekea Uingereza leo na kesho anatarajiwa kufanya vipimo vya afya baada ya hapo ni kusaini kandarasi ambayo itamueka ndani ya Manchester United mpaka mwaka 2029, Mshambuliaji huyo anatarajiwa kupewa mapumziko mafupi ndio ujiunge na wenzake kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu.

Acha ujumbe