Mokwena Aibukia Wydad Casablanca

Aliyekua kocha wa klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Rulani Mokwena amefanikiwa kujiunga na miamba ya soka kutoka nchini Morocco klabu ya Wydad Casablanca.

Kocha Mokwema amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuiongoza klabu ya Wydad Casablanca ambayo imekua haifanyi vizuri siku za hivi karibuni, Kocha huyo amekua kwenye muendelezo mzuri ndani ya kikosi cha Mamelodi Sundowns kabla ya kuamua kutimka klabuni hapo.mokwenaKocha huyo anategemewa kuirudisha klabu ya Wydad kwenye ubora wake ambao imekua nao kwa muda mrefu jambo ambalo linaonekana kutoweka siku za hivi karibuni, Hivo mwalimu huyo anatarajiwa kurejesha zama za mafanikio ndani ya miamba hiyo ya Morocco.

Kocha Rulani Mokwena amekua na mafanikio makubwa ndani ya Mamelodi Sundowns lakini hakufanikiwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani Afrika jambo ambalo linaelezwa kusababisha kuondoka ndani ya Mamelodi, Swali linabaki ni kama ataweza kushinda taji hilo na Wydad Casablanca.

Acha ujumbe