De Ligt Anaitaka United tu

Beki wa kimataifa wa Uholanzi Mathijjs De Ligt ambaye anakipiga klabu ya Bayern Munich inaelezwa ameipa kipaumbele klabu ya Manchester United pekee.

Beki De Ligt amemuambia wakala wake klabu pekee ambayo anaihitaji kucheza kuelekea msimu ujao ni Man United na mpaka sasa dili linakaribia kukamilika, Lakini vilabu kadhaa kama PSG vimeonesha nia ya kuhitaji saini ya beki huyo lakini beki huyo anataka kucheza Man Uited tu.de ligtMakubaliano baina ya mchezaji na klabu ya Man United yameshafikiwa siku kadhaa zilizopita kutokana na vyanzo mbalimbali nchini Ujerumani, Huku suala likibaki kwa vilabu baina ya Man United na Bayern Munich huku Bayern wakihita kiasi cha €50 milioni ili kumuachia beki huyo.

Mkataba wa miaka mitano ndio mkataba ambao anatarajiwa kusaini beki De Ligt kuitumikia Manchester United mpaka mwaka 2029, Kinachosubiriwa kwasasa ni Man United kulipa kiasi kinachohitajika na Bayern ili wampate mchezaji huyo na mpaka sasa mazungumzo yanaendelea vizuri.

Acha ujumbe