Manchester United ya Waholanzi

Manchester United ya Waholanzi ndio kauli ambayo unaweza kuielezea klabu hiyo kubwa kabisa barani ulaya kutokana na kile ambacho kinaendelea ndani ya klabu hiyo kwasasa.

Mpaka sasa klabu ya Manchester United inaongozwa na kocha wa kimataifa wa Uholanzi Erik Ten Hag huku benchi lake la ufundio pia likitawaliwa na Waholanzi, Kwani kocha msaidizi wa klabu hiyo Rene Hake nae ni raia wa Uholanzi bila kusahau aliyewahi kua mchezaji wa klabu hiyo Ruud Van Nistelrooy nae ni sehemu ya benchi la ufundi la klabu hiyo kuelekea msimu ujao.manchester unitedWakati huohuo klabu hiyo iko mbioni kukamilisha dili la wachezaji wawili ambao ni Joshua Zirkzee anayekipiga klabu ya Bologna, lakini pia Mathijjs De Ligt ambaye anakipiga ndani ya Bayern Munich wachezaji wote hawa wawili ni raia wa kimataifa wa Uholanzi.

Joshua Zirkzee ameshakubali kujiunga na klabu ya Man United na klabu hiyo imekubali kulipa kiasi cha pesa kinachohitajika na klabu ya Bologna, Hivo inaelezwa ndani ya wiki ijayo mchezaji huyo anaweza kutambulishwa kama mchezajin mpya wa mashetani wekundu.manchester unitedBeki Mathijjs De Ligt kwa upande wake yeye pia amekubali kujiunga na Manchester United tu licha ya klabu kama PSG kufukuzia huduma yake, Lakini mchezaji amesema ndio kwa Man United mpaka sasa na kuna kila dalili ya mchezaji huyo kujiunga na mashetani wekundu na ndio maana unaweza kusema Man united ya Waholanzi kwasasa.

Acha ujumbe