Manchester United Mbioni Kumalizana Zirkzee

Klabu ya Manchester United inaelezwa iko mbioni kumalizana na mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi ambaye anakipiga kwenye klabu ya Bologna Joshua Zirkzee.

Kocha Erik Ten Hag amekua kwenye mazungumzo ya simu mara kwa mara na Zirkzee akihitaji kupata saini yake kuelekea msimu ujao, Manchester United wapo kwenye mchakato wa kupindua meza kwa mshambuliaji huyo kwakua klabu ya Ac Milan nao wamekua karibu kupata saini ya mchezaji huyo.manchester unitedMashetani wekundu wao hawana tatizo na kulipa kiasi cha pesa ambacho klabu ya Bologna inakihitaji ambacho ni kiasi cha €40 milioni, Huku ikielezwa makubaliano yamebaki baina ya klabu ya Man United na wakala wa mchezaji Joshua Zirkzee anayefahamika kama Kia Joarbachian ambaye kulipwa kiasi fulani cha pesa.

Klabu ya Manchester United inahitaji kuhakikisha wanapata saini ya mchezaji huyo kwa namna yeyote, Kwani wanaelezwa wako tayari kulipa kiasi cha pesa kwa Bologna kiasi cha €40 milioni lakini pia wana uwezo wa kusubiri mwezi Agosti ambapo kiasi cha pesa ambacho Bologna wamekiweka kwenye mkataba ili kumuachia mchezaji huyo kitakua kimefika ukomo.

Acha ujumbe