Chelsea Yashusha Mashine

Klabu ya Chelsea imeendelea kufanya fujo sokoni baada ya kufanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji Renato Viega kutoka klabu ya Fc Basel ya nchini Ureno.

Chelsea imemsajili beki huyo wa kati raia wa kimataifa wa Ureno kwa dau la €14 milioni na kupewa mkataba mrefu wa miaka nane klabuni hapo mpaka mwaka 2032, Matajiri hao wa London wamekua wakitoa mikataba ya muda mrefu sana kwa wachezaji wao hivi karibuni.ChelseaBeki Renato Viega anasajiliwa baada ya matajiri hao wa London kushindwa katika dili la kumuwania beki wa kimataifa wa Italia Riccardo Calafiori ambaye mpaka sasa anaelekea klabu ya Arsenal, Beki Viega ana uwezo wa kucheza beki wa kati lakini pia ana uwezo wa kucheza kama beki wa pembeni.

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ulinzi baada ya kumsajili beki huyo wa kimatiafa wa Ureno mwenye umri wa miaka (21) ambaye anasifika kua na kipaji kikubwa, Lakini pia klabu hiyo itanufaika na beki huyo kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.

Acha ujumbe