Inter Milan Yamsajili Zielinski

Klabu ya Inter Milan mabingwa wa ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A wamefanikiwa kumsajili kiungo wa zamani wa klabu ya Napoli Piotr Zielinski.

Inter Milan katika kuhakikisha wanakiboresha kikosi chao wamemuongeza kiungo Zielnski kwenye eneo la kiungo katika kikosi chao kuelekea msimu ujao, Kiungo huyo wa kimataifa wa Poland amefanikiwa kujiunga na mabingwa hao wa Italia kwa uhamisho huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Napoli.inter milanMchezaji huyo baada ya kudumu ndani ya klabu ya Napoli kwa takribani miaka tisa amemua kutimka kwenye timu hiyo na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, Kiungo huyo ambaye ameitumikia Napoli tangu mwaka 2016 akitokea klabu ya Udinese hakusaini mkataba mpya ndani ya Napoli na kufanikiwa kuondoka kwa uhamisho huru.

Kiungo Zielinski mwenye umri wa miaka (30) anaenda kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Inter Milan kutokana na uzoefu ambao amekua nao, Kwani muda mrefu wa maisha yake ya soka ameutumikia ndani ya ligi kuu ya Italia hivo sio jambo gumu kwake kuanza maisha mapya ndani ya Nezzazuri.

Acha ujumbe