Van De Beek Kutimkia Girona

Kiungo wa klabu ya Manchester United Donny Van De Beek yuko mbioni kujiunga na klabu ya Girona ya nchini Hispania baada ya makubaliano ya vilabu vyote viwili.

Manchester United imekubali kumuuza Van De Beek kwa bei ndogo ya €5 milioni kwenda klabu ya Girona ikiwa ni baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi kushindwa kuonesha makali ndani ya klabu ya Man United, Huku majeraha yakiwa sehemu kubwa ya sababu ya kufeli kwa kiungo huyo ndani ya klabu hiyo.van de beekMakubaliano baina ya Man United na klabu ya Girona wameshakubaliana dau la kuweza kumpata kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi, Huku jambo linalosubiriwa ni maslahi binafsi baina ya mchezaji huyo na klabu ya Girona ambapo inaelezwa litajadiliwa wiki inayofuata.

Kiungo Donny Van De Beek amejiunga na Man United mwaka 2020 lakini hakufanikiwa kuonesha ubora mkubwa ndani ya kikosi hicho chini ya makocha takribani wanne, Klabu ya Man United imeona ni wakati sahihi wa kuachana na kiungo huyo kutokana na kushindwa kupata kile walichokitarajia.

Acha ujumbe