Alcantara Atundika Daluga rasmi

Kiungo wa kimataifa wa Hispania mwenye asili ya Brazil Thiago Alcantara ametangaza kuachana na mpira wa miguu leo hii akiwa na umri wa miaka (33) baada ya kuhudumu kwenye mpira wa miguu kwa muda mrefu.

Alcantara ameachana na mpira wa miguu rasmi huku klabu yake ya mwisho ikiwa ni Liverpool ya nchini Uingereza ambapo ametumika ndani ya klabu hiyo kwa takribani misimu mitatu, Mpaka sasa anaamua kutundika daluga licha ya kufukuziwa na timu nyingi kutoka nchini Saudia Arabia.AlcantaraKiungo huyo ambaye alianza soka ndani ya klabu ya Fc Barcelona akicheza kwa muda mfupi ambapo alitimkia klabu ya Fc Bayern Munich ya nchini Ujerumani ambapo alicheza kwa mafanikio makubwa, akitwaa mataji karibuni yote ambapo alibeba mataji (7) ya Bundesliga DFB Pokal mara (4)  Taji la ligi mabingwa ulaya (1) klabu bingwa ya dunia (1).

Mchezaji huyo ambaye alikua anatambulika kama moja ya viungo wenye ubora mkubwa kwenye kupiga pasi za aina zote fupi na ndefu, kuzuia, na kuchezesha timu zaidi akiifanya kazi hiyo kwa ufasaha akiwa ndani ya kikosi cha Bavarians ambapo alihudumu kwa takribani miaka saba yenye mafanikio makubwa.AlcantaraKiungo Thiago Alcantara anaachana na mpira akiwa na umri wa miaka (33) umri ambao wengi walitamani waendelee kumuona akisakata kabumbu kutokana na ubora na ufundi ambao alikua nao, Lakini majeraha ni moja ya sababu kubwa ambayo imechangia kiungo huyo kuachana na mpira wa miguu wakati huu kwani majeraha ya mara kwa mara yamekua yakimuandama sana.

Acha ujumbe