Alcantara Arejea Dimbani

Kiungo wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Hispania Thiago Alcantara anaelezwa amepona majeraha yaliyokua yanamsumbua na yuko tayari kuanza kuwatumikia majogoo hao wa Anfield.

Thiago Alcantara amekua akisumbuliwa na majeraha tangu msimu huu uanze lakini taarifa kutoka ndani ya Liverpool zimeeleza kua kiungo huyo yuko tayari sasa kuanza kuipambania jezi ya Liverpool kwenye michuano mbalimbali.alcantaraKlabu ya Liverpool ilikua na viungo kama Dominik Szoboszlai , Alexis Macallister,na Endo, Lakini bado huduma ya kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania imekua ikionekana inahitajika ndani ya kikosi cha Liverpool kutokana na ubora wa kiungo huyo.

Liverpool wameonekana kushindwa kutawala mchezo katika michezo kadhaa ya ligi kuu ya Uingereza na michuano mingine msimu huu, Huku ikionekana ni kutokana na kukosekana kwa kiungo mwenye uwezo wa namna hiyo lakini kurejea kwa Thiago kutaenda kutibu tatizo hilo.alcantaraKurejea kwa Thiago Alcantara ni wazi anaenda kuongeza ubora kwenye kikosi cha Liverpool ambao ndio vinara wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini pia ataisaidia timu hiyo kupata mzunguko sahihi wa wachezaji wenye ubora kwani Liverpool kwasasa wana viungo wanaofanya vizuri lakini kuwepo kwa Mhispania huyo kutawaimarisha zaidi.

Acha ujumbe