Manchester United Ngoma Nzito Mbele ya Bayern

Klabu ya Manchester United leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Fc Bayern Munich katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya ambao ukakwenda kuamua hatma ya klabu hiyo kwenye michuano ya ulaya msimu huu.

Manchester United wanahitaji kushinda mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Fc Bayern Munich ili kujihakikishia kuwepo kwenye hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa ulaya, Au kuendelea kuwepo kwenye michuano ya ulaya kwa ujumla.manchester UnitedKwenye kundi A ambalo Man United wapo mpaka sasa wanashika mkia kwenye kundi hilo wakiwa wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu, Huku wakipoteza michezo mitatu wakiwa na kusuluhu mchezo mmoja hivo wana alama nne mpaka sasa.

Jambo ambalo linafanya mchezo huu kua mgumu sana ni kwasababu Man United watahitajika kushinda mchezo dhidi ya Bayern Munich, Lakini wakati huohuo watapaswa kuombea sare mchezo kati ya Galatasaray na Fc Copenhagen kumalizika kwa sare ili wao waweze kufuzu hatua ya 16 bora.manchester UnitedManchester United wakishinda mchezo wa leo dhidi ya Bayern Munich watakua wamejihakikishia kubaki kwenye michuano ya ulaya, Kwani hatakama hawatafuzu hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa ulaua lakini watafanikiwa kwenda michuano ya Uefa Europa league wakiwa na alama zao saba endapo mchezo wa Galatasaray na Copenhagen utatoa mshindi.

Acha ujumbe