Manchester United Yawapiga Pini Waandishi

Klabu ya Manchester United imeeleza kua imewapiga marufuku baadhi ya waandishi na vyombo vya habari nchini Uingereza kutokana na kuchapisha habari bila kuwasiliana na klabu.

Manchester United imeweka wazi kua hawajapiga marufuku vyombo vya habari kutokana na kuchapisha habari ambazo hawazipindi, Lakini wamezuia hali hiyo kutokana na kuchapisha habari hizo kiholela.manchester UnitedKumekua na mlipuko wa habari za ndani za klabu hiyo mara kwa mara ambazo klabu hiyo haipendezwi nazo, Hivo imewataka waandishi na vyombo vya habari kabla ya kuchapisha habari zao wawasiliane na uongozi wa klabu ili kupata ridhaa.

Hivi karibuni kumekua na habari zinazohusu kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag kupoteza nguvu ya ushawishi klabuni hapo, Hii ni moja ya habari ambayo inaeleza kuchukiza uongozi wa klabu ya Man United na kupelekea kuwachukulia hatua baadhi ya vyombo vya habari.manchester UnitedLengo la klabu ya Manchester United kuwachulia hatua baadhi ya waandishi na vyombo vya habari vinavyochapisha habari bila kuwasiliana na klabu hiyo ni kuhakikisha wanazuia kusambaa kwa habari ambazo zinazua taharuki klabuni na kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Acha ujumbe