Newcastle Kuingia Sokoni Kutafuta Golikipa

Klabu ya Newcastle United watalazimika kuingia sokoni kwenye dirisha dogo la mwezi Januari kwajili ya kusajili golikpa mpya atakaevaa viatu vya Nick Pope aliyepata majeraha.

Golikipa Nick Pope amepata meraja ya bega ambayo yatamueka nje kwa muda wa miezi minne, Hivo klabu ya Newcastle watahitaji kutafuta golikipa mwingine mwenye ubora mkubwa kwajili ya kumrithi Pope.newcastleGolikipa Nick Pope alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza Jumamosi dhidi ya Manchester United na kupelekea bega lake kuumia na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje kwa muda wa miezi minne.

Klabu hiyo ambayo inafanya vizuri kwasasa ndani ya ligi kuu ya Uingereza na golikipa Nick Pope amekua moja ya mchezaji muhimu sana ndani ya timu hiyo, Hivo watahitaji golikipa mwingine mwenye ubora ambae ataweza kuonyesha ubora kama Nick Pope.newcastleKlabu ya Newcastle wanahusishwa na golikipa wa zamani wa klabu ya Manchester United ambaye hana timu mpaka wakati huu, Lakini pia wakihusishwa na golikipa raia wa kimataifa wa Uingereza anayekipa klabu ya Arsenal Aaron Ramsdale ambaye anaonekana kupoteza nafasi klabuni hapo.

 

Acha ujumbe