Klabu ya Manchester United ipo mawindoni kuhakikisha inapata saini ya beki raia wa kimataifa wa kireno Antonio Silva anayekipiga klabu ya Benfica ya nchini Ureno.
Manchester United imemfanya kipaumbele beki huyo mwenye umri wa miaka 20, Kati ya mabeki wote wa kati ambao wamekua wakiwafatilia tangu dirisha kubwa lililopita.
Klabu hiyo ina mpango wa kuingia sokoni kwenye dirisha dogo la mwezi Januari kwajili ya kutafuta beki wa katikati haswa anaetumia mguu wa kulia, Huku Antonio Silva akiwa ndio kipaumbele zaidi ya wengine.
Mabeki wengine kama Jean Clair Todibo, na Edmond Tapsoba wanaendelea kuwepo kwenye orodha ya mabeki wanaohitajika na klabu hiyo, Lakini kipaumbele ni wazi ni beki huyo wa kimataifa wa Ureno.
Klabu ya Manchester United inamtolea macho Antonio Silva kutokana umri mdogo wake aliokua nao, Lakini uwezo ambao amekua akiuonesha ndani ya Benfica pia umewavutia mashetani hao wekundu na kumuweka kama kipaumbele chao kwa upande wa mabeki.

