Kutokana na Jeraha alilolipata Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Yanga kwenye mchezo wao dhidi ya Al Ahly Joyce Lomalisa ameshindwa kusafiri na timu kwenda Ghana kuwavaa MEDEAMA
Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu ya Yanga Ali kamwe ni alisema kwamba Lomalisa ataukosa mchezo wa Ijumaa wa Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini dhidi ya MADEAMA Utakaochezwa nchini Ghana.Na nafasi yake itakuchukuliwa na Nickson Kibabage ambaye aliingia kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Lomalisa ambaye alipata majeraha katika mchezo huo.
Ni wazi kua klabu ya Yanga itakua na pengo kuelekea mchezo wao wa tatu katika ligi ya mabingwa Afrika, Kwani beki huyo raia wa kimataifa wa Congo amekua na kiwango bora sana klabuni hapo.