Chiellini Astaafu Soka Rasmi

Beki raia wa kimataifa wa Italia Giorgio Chiellini ametangaza kustaafu soka rasmi akiwa na umri wa miaka 39 ndani ya klabu ya Los Angeles Lakers baada ya kuutumikia mchezo huo kwa muda mrefu na mafanikio ya kutosha.

Giorgio Chiellini  aliibukia katika klabu ya Livorno ya daraja la pili nchini Italia kabla ya kucheza vilabu vya As Roma, Fiorentina, na baadae kujiunga na klabu ya Juventus ambayo amedumu kwa muda mrefu sana na kupata mafanikio makubwa.chielliniBeki huyo raia wa kimataifa wa Italia anahesabika kama moja ya mabeki mahiri kuwahi kutokea duniani, Kwani ameweza kudumu kwa muda mrefu sana katika kiwango cha akicheza kwenye kiwango cha juu kwa takribani miaka 14.

Beki huyo pia alifanikiwa kushinda mataji kadhaa akiwa na klabu ya Juventus ambayo ndio amedumu kwa muda mrefu zaidi,akifanikiwa kushinda ligi kuu ya Italia mara tisa, Coppa Italia mara tano, Supercoppa Italiana mara tano, Bila kusahau mshindi wa pili ligi ya mabingwa ulaya mara mbili.chielliniKatika ngazi ya timu ya taifa Giorgio Chiellini amefanikiwa kufanikiwa akiwa na timu ya taifa ya Italia ambapo ameitumikia kwa muda mrefu vilevile, Mwaka 2012 alikua kwenye kikosi cha Italia kilichocheza fainali ya michuano ya Euro na kupoteza mbele ya Hispania lakini mwaka 2021 akiwa kama nahodha aliiongoza Italia kutwaa taji hilo akiwa kama nahodha.

Acha ujumbe