Reece James Nje Mpaka Mwezi March

Beki na nahodha wa klabu ya Chelsea Reece James amefanyiwa vipimo na jopo la madaktari wa klabu hiyo na kufahamika anasumbuliwa na misuli ya paja baada ya kushindwa kumaliza mchezo siku ya Jumapili dhidi ya Everton.

Reece James amepata majeraha ya misuli ya paja na kumfanya kukaa nje ya uwanja kwa muda unaokadiriwa kama miezi mitatu, Kwani inaelezwa mchezaji huyo atarejea uwanjani mwezi wa tatu mwaka 2024.reece JamesBeki huyo alishindwa kuendelea na mchezo siku ya Jumapili akitoka dakika ya 26 ya mchezo kutokana na majeraha aliyoyapata, Huku leo ikitoka taarifa rasmi ya majeraha ambayo yanamkabili na atakaa nje ya uwanja kwa muda gani.

Nahodha huyo wa klabu ya Chelsea amekua akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara kwani hata msimu huu hii sio mara ya kwanza kupata majeraha amewahi kupata majeraha msimu huu pia na amerejea kutoka kwenye majeraha hivi karibuni.reece JamesReece James amekua akikosekana mara kwa mara ndani ya klabu hiyo na timu ya taifa ya Uingereza kutokana na majeraha, Klabu hiyo imetafuta mbadala wa mchezaji huyo kwa kumsajili Malo Gusto kutoka Olympique Lyon katika majira ya joto yaliyopita.

 

Acha ujumbe