Beki wa kulia na nahodha wa klabu ya Chelsea Reece James amepata mejaraha tena katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Everton katika dimba la Goodson Park.
Reece James amepata majeraha na ameshindwa kuendelea na mchezo kwani ametolewa dakika ya 26 ya mchezo katika mchezo wao unaoendelea dhidi ya klabu ya Everton.Taarifa rasmi hazijatoka mchezaji huyo atakaa nje ya uwanja kwa muda gani kutokana na majeraha aliyoyapata leo pia hayajafanyiwa uchunguzi na jopo la madaktari wa klabu ya Chelsea.
Beki huyo amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara na hata msimu huu tayari ameshapata majeraha mara kadhaa,Hii imekua changamoto kwa beki huyo ambaye amekua mchezaji tegemeo klabuni hapo kwa misimu kadhaa.Mara kadhaa klabu ya Chelsea imekua ikipata wakati mgumu kutokana na kukosa hudumu ya Reece James ambaye amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara, Huku ikielezwa ndio sababu ya Chelsea kuingia sokoni kufanya usajili wa beki Malo Gusto kutoka Olympique Lyon.