Klabu ya soka ya Simba inachechemea kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya jana kukubali kipigo cha bao moja kwa bila mbele ya Wydad Casablanca.
Klabu ya Simba sasa inakua na wakati mgumu katika kundi B ambapo mpaka sasa inashika mkia ikiwa ina alama mbili baada ya kucheza michezo mitatu ikiwa zinawaweka kwenye mazingira magumu kufuzu hatua ya robo fainali.Wekundu wa Msimbazi wanakua kwenye wakati mgumu kwani wanapaswa kushinda michezo yao mitatu inayofuata ili kujihakikishia kufuzu hatua ya robo fainali kutokana na msimamo ulivyo mpaka sasa.
Mchezo ujao Wekundu wa Msimbazi watakua nyumbani kumenyana na Wydad Casablanca, Hivo ili kukufua matumaini ya kwenda hatua ya robo fainali wanapaswa kupata matokeo katika mchezo huo kabla ya kucheza na Asec Mimosas na kumaliza nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy.Simba wanapaswa kushinda michezo yao iliyobaki ambayo ni mitatu na watakua wamejihakikishia kufuzu hatua ya robo fainali, Lakini matokeo ya tofauti watakayoyapata katika michezo hiyo watapaswa kusubiria matokeo watakayoyapata wapinzani wao.