Tottenham Yamuongezea Mkataba Udogie

Klabu ya Tottenham Hotspurs imefikia makubaliano ya kumuongezea mkataba beki wake wa kushoto raia wa kimataifa wa Italia Destiny Udogie baada ya mazungumzo ya muda mrefu baina ya klabu na mchezaji huyo.

Beki Udogie mwenye umri wa miaka 21 amekubali kusaini mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya klabu ya Tottenham kwa muda mrefu zaidi, Kwani mchezaji huyo ataendelea kusalia kwenye viunga vya klabu hiyo mpaka mwaka 2029.TottenhamMchezaji huyo amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Spurs chini ya kocha Ange Postecoglou, Hii ikiwa moja ya sababu za beki huyo kuongezewa mkataba ndani ya timu hiyo kwakua ni chaguo la mwalimu.

Beki Destiny Udogie ameongeza mkataba mpaka mwaka 2029 wakati huo kukiwa na kipengelea cha kuongeza mwaka mwingine mmoja, Hivo kimahesabu mchezaji huyo anaweza kusalia ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2030.TottenhamKlabu ya Tottenham Hotspurs wapo kwenye mradi wa muda mrefu wakihitaji kutengeneza timu ambayo itakua na ubora kwa muda mrefu, Huku ikiwa ndio sababu ya kuhakikisha wanawaongezea mikataba wachezaji vijana kama Udogie klabuni hapo kwajlili ya mipango ya muda mrefu.

Acha ujumbe