Klabu ya Tottenham imeweka wazi haina mpango wa kumuachia kiungo wake raia wa kimataifa wa Denmark Pierre Emile Hojbjerb ambaye amekua akifukuziwa na vilabu mbalimbali.
Vilabu mbalimbali vimekua vikifukuzia huduma ya kiungo Pierre Emile Hojbjerg kama Juventus na Ajax, Lakini Tottenham wameweka wazi hawana mpango wa kumuachia kiungo huyo kwa mkopo katika dirisha dogo la mwezi Januari.Kiungo Pierre Emile Hojbjerg amekua sio chaguo la kwanza la mwalimu mpya Ange Postecoglou jambo ambalo lilimfanya pia kiungo kufikiria kuondoka klabuni hapo, Lakini kutokana na muenendo wa majeraha wa wachezaji klabuni hapo kiungo huyo hataruhusiwa kuondoka klabuni hapo.
Klabu ya Tottenham mpaka sasa imeshakataa ofa ya klabu ya Atletico Madrid kutoka nchini Hispania ambao walikua wanahitaji huduma ya mchezaji huyo kwenye majira ya baridi mwezi Januari.Pierre Emile Hojbjerg ataendelea kuwepo ndani ya Spurs kwakua klabu hiyo haina mpango wa kumtoa kwa mkopo katika dirisha dogo la mwezi Januari, Huku jambo hili likichagizwa zaidi na wimbi la mejeruhi ambalo linaendelea kuiandama klabu hiyo.