Tottenham Yapigwa Tena

Klabu ya Tottenham imekubali kichapo kwenye mechi ya pili mfululizo msimu huu baada ya kupoteza Jumatatu dhidi ya Chelsea leo wamekubali kichapo tena mbele ya Wolves.

Klabu ya Wolves wakiwa nyumbani katika dimba lao la Molineux walifanikiwa kutoka nyuma na kuifunga klabu ya Tottenham kwa mabao mawili kwa moja katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.TottenhamMajogoo wa hao kutoka jiji la London walifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa kinda wao Brennan Johnson mapema tu dakika ya tatu ya mchezo goli lilidumu mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza Spurs wakionekana wakihitaji kupata goli la pili ili kujihakikishia ushindi katika mchezo huo, Lakini klabu ya Wolves nao walionekana kufika katika lango la Spurs mara kwa mara wakitafuta bao la kusawazisha.TottenhamJitihada za Wolves kutafuta bao la kusawazisha zilifanikiwa ambapo dakika ya 90 mchezaji alietokea benchi Pablo Sarabia alifunga bao la kusawazisha, Wakati Tottenham wakiwa hawajaa sawa baada ya kusawazishiwa bao dakika ya 97 Mario Lemina alipiga msumari wa pili na kuizamisha meli ya Spurs na kukubali kuacha alama zote tatu kwa Wolves.

Acha ujumbe