MATAJIRI wa Dar, Azam FC wameendelea kujikita kuwa namba moja kwenye msimamo baada ya kukomba ponti tatu mbele ya JKT Tanzania.
Kwenye mchezo uliochezwa Desemba 11 2023 Uwanja wa Azam Complex unakuwa ni ushindi wa tano mfululizo ndani ya Ligi Kuu Bara
Mabao ya Azam FC yalifungwa na Sospeter Bajana dakika ya kwanza likawekwa usawa na Najimu Magulu dk ya 37.Mwisho ngoma ilisoma Azam FC 2-1 JKT Tanzania ukiwa ni moja ya mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.
Jioni kabisa Idd Suleiman Nado akapachika bao la ushindi dakika ya 84 pointi tatu zikabaki Azam Complex.
Ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 12 wanafuatiwa na Yanga walio nafasi ya pili na ile ya tatu ipo kwa Simba.