Greenwood Kurejea United Kesho

Winga wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood ni rasmi kesho atarejea kwenye kikosi cha Man United baada ya miaka mitatu ya kua nje ya klabu hiyo.

Winga huyo ameripotiwa atarejea kwenye kiwanja cha mazoezi na wachezaji wengine ambao watajumuika kuanza mazoezi ya klabu hiyo kesho kujiandaa na msimu mpya, Winga Greenwood tangu mwaka 2021 apate kesi ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2021 hakuwahi kurejea ndani ya klabu hiyo.greenwoodMsimu uliomalizika winga huyo aliitumikia klabu ya Getafe ya nchini Hispania akionesha ubora mkubwa klabuni hapo lakini mkopo wake umemalizika na amerejea kwenye klabu yake iliyomkuza, Huku kesho itakua ni mara kwanza ya yeye kukanyaga nyasi za uwanja wa mazoezi wa klabu ya Man United unaofahamika kama Carrington.

Winga huyo wa kimataifa wa Uingereza yupo kwenye mipango ya kuuzwa ndani ya klabu hiyo kama taarifa zilivyoeleza hapo awali, Lakini Man United wanahitaji kiwango kizuri cha pesa ambacho kitawashawishi kumuuza winga huyo na kama hawatapata dau zuri basi kuna uwezekano mchezaji huyo akabaki ndani ya klabu.greenwoodMashabiki wengi wa klabu ya Manchester United wanaonesha kua wanatamani sana kumuona Greenwood akipewa nafasi ya pili ndani ya klabu hiyo licha ya kosa alilolifanya miaka mitatu iliyopita mpaka sasa klabu imeshikilia msimamo wa kumuuza mchezaji huyo, Lakini kiu ya mashabiki wengi wa klabu hiyo ni kumuona mchezaji huyo akiwa na jezi za klabu ya Man United kwa mara nyingine.

Acha ujumbe