Southgate Aachia Ngazi Uingereza

Aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate ametangaza kuachana na kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza ambacho amehudumu kwa takribani miaka nane.

Southgate amefanikiwa kuiongoza timu ya taifa ya Uingereza tangu mwezi Septemba mwaka 2016 akichukua nafasi kwa kocha Sam Allardyce ambaye alijiuzulu nafasi hiyo, Hivo kocha huyo ambaye alikua kocha wa vijana wa timu ya taifa ya Uingereza akachukua majukumu hayo mapya.southgateKocha huyo ameachana na timu hiyo baada ya kuiongoza kwenye michuano mikubwa minne ambayo ni kombe la dunia 2018 ambapo walicheza nafasi ya mshindi wa tatu, 2021 kwenye michuano ya Euro wakipoteza fainali, 2022 kombe la dunia wakitolewa hatua ya robo fainali, huku michuano yake ya mwisho ni Euro 2024 ambapo wamepoteza fainali mbele ya timu ya taifa ya Hispania siku ya jumapili.

Chama cha soka cha Uingereza (FA) bado hakijaeleza ni kocha gani ambaye ataifundisha timu yao ya taifa baada ya kocha huyo kuachia ngazi kwenye kikosi chao, Japokua wiki iliyopita ilielezwa FA wana mpango wa kumuongezea mkataba kocha Gareth bila kuzingatia matokeo ya fainali yatakuaje.southgateIkumbukwe kabla ya michuano ya Euro mwaka 2024 kocha Southgate aliweka wazi ataachana na kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza, Lakini taarifa zilizoshtua ni FA kutaka kumuongezea mkataba ili mpaka sasa ni wazi chama hicho soka kimeshindwa kumshawishi kocha huyo kubakia kwenye timu hiyo kutokana na maamuzi aliyoyafanya mapema leo.

Acha ujumbe