Mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano kati ya Simba SC na Yanga SC unatarajiwa kupigwa usiku wa leo saa 2:15 uwanja wa new Amani Complex, huku maandalizi yakiendelea kukamilishwa kuelekea kwenye mtanange huo muhimu katika kalenda ya soka nchini Tanzania.
Shirikisho la soka visiwani Zanzibar ZFA limethibitisha kuwa mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi kutoka Kenya, Dickens Mimisa Nyagrowa, ambaye amepata nafasi ya kusimamia fainali hiyo kutokana na uzoefu wake katika mechi za kimataifa. Uamuzi huo unalenga kuhakikisha mchezo unachezwa kwa haki na viwango vya juu vya usimamizi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika upande wa waamuzi wasaidizi, mwamuzi msaidizi namba moja atakuwa Ali Mbwana kutoka Zanzibar, huku msaidizi namba mbili akiwa ni Yusuf Shombe, pia kutoka Zanzibar. Waamuzi hawa wanatarajiwa kutoa msaada muhimu kwa mwamuzi mkuu kuhakikisha sheria za mchezo zinafuatwa kikamilifu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwamuzi wa akiba katika mchezo huo atakuwa Ishaka Mwalile kutoka Dar es Salaam. Huyu atakuwa tayari kuchukua majukumu endapo kutatokea dharura yoyote kwa waamuzi walioko uwanjani.
Fainali hiyo ya Kombe la Muungano kati ya Simba na Yanga inatarajiwa kuvuta hisia kubwa za mashabiki nchini na nje ya mipaka ya Tanzania kutokana na ukubwa wa timu hizi mbili. Usimamizi wa waamuzi kutoka mataifa tofauti unalenga kuongeza uaminifu na ushindani wa haki katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka.

