Mshambuliaji wa Harry Kane amesema ana imani kubwa kuwa Bayern Munich wanaweza kufuzu fainali ya UEFA Champions League licha ya kupoteza kwa mabao 5-4 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa Ufaransa.
Bayern walionekana kuzidiwa kabisa baada ya PSG kufunga mabao mawili ndani ya dakika mbili mwanzoni mwa kipindi cha pili na kufanya matokeo kuwa 5-2. Hata hivyo, mabao ya Dayot Upamecano na Luis Díaz ndani ya dakika tatu yaliwarudisha kwenye mchezo kwa kupunguza pengo hadi 5-4, hali iliyoongeza matumaini kuelekea mchezo wa marudiano nchini Ujerumani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza baada ya mchezo, Kane alisema ushindi utategemea nani atatumia vizuri nafasi katika mechi ijayo.“Itakuwa ni nani atakayetumia vizuri nafasi zake wiki ijayo. Kulikuwa na nafasi nyingi leo, na naamini hali itakuwa hiyo hiyo kwenye mechi ijayo,” alisema Kane.
Kane, aliyefunga bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti dakika ya 17, alisisitiza umuhimu wa mashabiki katika mchezo wa marudiano.“Tutakuwa nyumbani na mashabiki wetu watakuwa nyuma yetu, tunaamini hilo linaweza kutusaidia kuvuka hatua hii,” aliongeza.
Licha ya kuwa nyuma kwa mabao matatu, Kane alisema timu yake ilionyesha moyo mkubwa wa kupambana.“Tunaheshimu sana jinsi tulivyorejea kutoka 5-2 hadi 5-4. Kuwa ugenini na kuwa nyuma kwa namna hiyo ni hali ngumu, lakini tulipambana na bado tupo kwenye mashindano,” alisema.
Nahodha huyo wa England pia aliweka rekodi mpya kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa England kufunga katika mechi sita mfululizo za Champions League, akifikisha mabao 13 msimu huu.“Tulikuwa na nafasi za kumaliza mchezo mapema, lakini hatukutumia vizuri pasi za mwisho na umaliziaji,” alieleza.
Kwa upande mwingine, Kane alisifu kiwango cha juu cha mchezo huo, akieleza kuwa ulikuwa ni pambano la timu mbili bora barani Ulaya.“Tuliona timu mbili za kiwango cha juu, hasa katika mashambulizi, kasi na nguvu ya mchezo. Ilikuwa ni vita ya kweli kati ya timu mbili kubwa,” alihitimisha.

