Klabu ya Simba SC inatajwa kuwa katika mazungumzo ya kumsajili kipa wa timu ya taifa ya Nigeria, Stanley Nwabali, katika jitihada za kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao.
Nwabali alionyesha kiwango cha juu katika michuano ya AFCON 2025 iliyofanyika Morocco, hali iliyovutia klabu kadhaa barani Afrika, huku kwa sasa akikipiga katika klabu ya Chippa United.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Taarifa zinaeleza kuwa Simba wanachunguza uwezekano wa kuongeza nguvu eneo la golini licha ya kuwa tayari na makipa wawili wa kigeni, Djibrilla Kassali na Moussa Camara.
Iwapo usajili huo utakamilika, unatarajiwa kuongeza ushindani mkubwa ndani ya kikosi hicho, jambo ambalo linaweza kuathiri nafasi za baadhi ya makipa waliopo kwa sasa.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna uthibitisho rasmi uliotolewa na Simba SC kuhusiana na taarifa hizo za mazungumzo.

