Winga nyota wa Paris Saint-Germain, Khvicha Kvaratskhelia, amesema ana matumaini ya kuitia hamasa timu yake kufika fainali ya UEFA Champions League kwa mara nyingine, kuelekea nusu fainali dhidi ya Bayern Munich.
Nyota huyo wa Georgia, maarufu kwa uwezo wake wa kupenya na kuwachambua mabeki, amesema anafurahia kucheza soka na kuamini anaweza kuisaidia PSG kupata matokeo mazuri barani Ulaya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza kabla ya mchezo huo, alisema, “Ninacheza soka kwa sababu ninaipenda, na kila mara ninafurahia kuwa uwanjani. Ni muhimu pia kufanya mambo mazuri na ya kuvutia kwa mashabiki.”
Kvaratskhelia, aliyejiunga na PSG akitokea SSC Napoli, amekuwa na msimu bora akiwa na mabao 15 katika mashindano yote, huku nane kati ya hayo yakitoka katika Ligi ya Mabingwa.
Kocha wa PSG, Luis Enrique, ameonyesha imani kubwa kwa mchezaji huyo, huku akisema, “Ligi ya Mabingwa ina nguvu ya kipekee—inaleta hamasa kwa wachezaji na kila mmoja anataka kufanya vizuri katika hatua hizi.”
PSG wanatarajia kumtumia Kvaratskhelia pamoja na Ousmane Dembélé katika mchezo huo muhimu, wakilenga kupata ushindi wa kwanza kabla ya marudiano yatakayochezwa Ujerumani.

