Klabu ya Manchester United imekaribia kufuzu kwa UEFA Champions League msimu ujao baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford F.C. katika mchezo wa kusisimua wa Ligi Kuu England uliochezwa Old Trafford.
Mchezo ulianza kwa kasi ambapo Kobbie Mainoo alionyesha ustadi mkubwa kabla ya kumpasia Amad Diallo, lakini juhudi hiyo ilizuiwa na beki Sepp van den Berg akiwa mstari wa goli.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 11 kupitia Casemiro aliyemalizia pasi ya Harry Maguire iliyotokana na krosi ya Bruno Fernandes, huku Benjamin Šeško akiongeza la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Akizungumzia ushindi huo, nahodha Bruno Fernandes alisema, “Tulihitaji ushindi huu muhimu na tumefanya kazi kubwa kama timu kuhakikisha tunabaki kwenye mbio za kufuzu Ligi ya Mabingwa.”
Kipindi cha pili kilishuhudia Brentford wakiongeza presha, na Mathias Jensen alifunga bao la kufutia machozi dakika ya 87, lakini haikutosha kuzuia ushindi wa United.
Kwa matokeo hayo, Manchester United sasa wanakaribia kufuzu Ligi ya Mabingwa na wanaweza kuthibitisha hilo watakapokutana na Liverpool F.C. katika mchezo ujao, huku Brentford wakiendelea kusaka nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya.

