Luis Enrique, kocha wa mabingwa watetezi wa Paris Saint-Germain, amemwaga sifa kwa wapinzani wao Bayern Munich kuelekea mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League utakaochezwa kesho.

“Vincent Kompany ni kocha wa kiwango cha juu; tayari amethibitisha hilo nchini Uingereza. Tumeona jinsi ilivyo ngumu kucheza dhidi yao. Wao ni miongoni mwa timu ninazopenda kuzitazama. Daima wanashambulia na wanafunga idadi kubwa ya mabao ya kushangaza. Ni furaha kubwa kutazama timu kama hiyo.” Alisema Mhispania huyo.
Alipoulizwa moja kwa moja kuhusu winga Michael Olise, kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 alijibu:
“Ninawapenda wachezaji wote wa Bayern Munich sio Michael Olise tu, bali kila mmoja wao. Wameonyesha ubora wao. Alipoulizwa ni nani kiini cha kikosi cha Munich, alitaja wachezaji wengi akisema: “Kimmich, Harry Kane, Jamal Musiala, Olise, Luis Díaz, Laimer, Dayot Upamecano, Tah, Manuel Neuer, Stanisic wote, timu nzima. Ndiyo, wana nyota, lakini muhimu zaidi ni timu.”
Enrique alitabiri “mchezo wa kuvutia kwa kila mtu”, huku mabingwa watetezi PSG wakiwa na imani kubwa.
Wako katika kiwango kizuri sana, Katika mechi kama hizi, mambo madogo ndiyo huamua, hivyo lazima wawe tayari kwa kila hali. Wana imani, lakini wanajua pia itakuwa kazi ngumu.

Luis Enrique alisema kuwa wakiwa na wachezaji wake wote muhimu wakiwa fiti kwa mechi za maamuzi, kocha huyo alisema:
“Hicho ndicho uchawi wa UEFA Champions League; kila mtu anataka kuwa sehemu yake, na hilo linakupa nguvu maalum huku azma hiyo ikiungwa mkono na Khvicha Kvaratskhelia.
“Bayern Munich wako katika kiwango kizuri, lakini nasi pia tuko vizuri. Tunaweza kufanikisha lolote na kumshinda yeyote.”
Pia alionyesha heshima kubwa kwa kipa nahodha wa Bayern Manuel Neuer, akimuita mmoja wa makipa bora duniani. Ni gwiji, na tunajua uwezo wake.


