Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé, yuko hatarini kuukosa mchezo wa El Clasico utakaopigwa Mei 10 baada ya klabu yake kuthibitisha kuwa amepata jeraha la paja.
Katika taarifa rasmi, Madrid walisema: “Amegundulika kuwa na jeraha kwenye misuli ya semitendinosus ya mguu wake wa kushoto,” baada ya nahodha huyo wa Ufaransa kutolewa uwanjani akiwa ameumia katika sare ya 1-1 dhidi ya Real Betis kwenye La Liga Ijumaa iliyopita.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Awali, mabingwa hao wa Ulaya walidokeza kuwa Mbappe alikuwa na uchovu wa misuli, lakini vipimo vya ziada vilibaini kuwa mshambuliaji huyo kinara wa mabao ameumia rasmi.
Real Madrid, ambao wapo nafasi ya pili La Liga wakiwa nyuma kwa pointi 11 dhidi ya vinara FC Barcelona, wanatarajiwa kucheza dhidi ya RCD Espanyol Jumapili kabla ya kukutana na wapinzani wao wakubwa katika El Clasico wiki inayofuata.
Iwapo Madrid watapoteza pointi dhidi ya Espanyol bila Mbappe na Barcelona wakaifunga CA Osasuna, kikosi cha kocha Hansi Flick kitathibitishwa kutwaa ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo.
Mbappe, mwenye umri wa miaka 27 na bingwa wa dunia 2018, amekuwa akisumbuliwa na majeraha msimu huu, hali inayozua wasiwasi nchini Ufaransa kuelekea Kombe la Dunia litakaloanza Juni 11 nchini Marekani, Canada na Mexico, ambapo aliwahi kukiri kuwa changamoto zake za kiafya zimemsababishia “msongo wa mawazo, hasira na hofu.”

