Kiungo wa Xavi Simons wa klabu ya Tottenham Hotspur amethibitisha kuwa ataukosa msimu uliosalia pamoja na FIFA World Cup 2026 baada ya kupata jeraha kubwa la goti (ACL). Simons alipata jeraha hilo katika ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers, baada ya kuanguka vibaya kufuatia mpambano na beki Hugo Bueno.
Vipimo vya kitabibu vilithibitisha kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi amechanika kano la goti kwenye goti la kulia, jeraha linalotarajiwa kumuweka nje ya uwanja kwa takribani miezi 12. Hali hiyo inamaanisha kuwa hataweza kushiriki Kombe la Dunia lijalo litakalofanyika Canada, Mexico na Marekani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Simons alielezea maumivu yake kufuatia tukio hilo. “Wanasema maisha yanaweza kuwa magumu, na leo ndiyo nahisi hivyo. Msimu wangu umefika mwisho ghafla na bado najitahidi kuelewa kilichotokea. Kwa kweli nimevunjika moyo. Nilichotaka ni kuipigania timu yangu, lakini sasa nimepoteza nafasi hiyo… pamoja na ndoto ya Kombe la Dunia,” alisema Simons.

Kocha wa Spurs, Roberto De Zerbi, alieleza kuwa alizungumza na mchezaji huyo mara baada ya tukio hilo na kumpa faraja. “Niliongea naye na kwa sasa anajisikia nafuu kidogo ukilinganisha na alipoumia,” alisema kocha huyo baada ya mchezo.
Kabla ya jeraha hilo, Simons alikuwa ameanza kurejea katika kiwango chake bora, akifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao katika michezo mitano ya mwisho. Tangu ajiunge na Spurs akitokea RB Leipzig kwa ada inayokadiriwa kufikia euro milioni 65, amecheza mechi 28 za Ligi Kuu England akifunga mabao mawili na kutoa pasi tano za mabao.
Jeraha hilo linaongeza presha kwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, Ronald Koeman, kuelekea Kombe la Dunia. Wachezaji kadhaa muhimu akiwemo Frenkie de Jong, Memphis Depay na Matthijs de Ligt wamekuwa wakikabiliwa na majeraha, huku wengine wakikosa mechi za kirafiki za hivi karibuni. Uholanzi imepangwa Kundi F pamoja na Japan, Sweden na Tunisia, na itaanza kampeni yake dhidi ya Japan Juni 14.

