Hatimaye pazia la ligi kuu ya NBC Tanzania linaenda kuzinduliwa hii leo kwa mchezo mmoja ambapo wenyeji Pamba Jiji ambao wamepanda daraja msimu huu watakiwasha dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 10:00 jioni ambapo Prisons msimu uliopita, alishika nafasi ya 9 kati ya timu 16 huku timu hiyo kutoka jijini Mbeya ikiwafunga Wekundu wa Msimbazi msimu uliopita.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Pamba Jiji wao baada ya miaka 23 iliyopita kushuka daraja na sasa wapo ligi kuu kupambania taji, huku timu hiyo ikiwa chini ya Goran Kopuvonic wanaanza kibarua chao dhidi ya Wajelajela ambao wanapewa nafasi kubwa kushinda leo.


