Leonel Ateba Aipiga Simba Mil 600 tzs, Mashine ya Ubaya Ubwela

KLABU  YA SIMBA Imetambulisha kifaa kipya, Straika Leonel Ateba kutoka USM Alger ya Algeria ili kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Wekundu iliyopo chini ya kocha Fadlu Davids aliyehitaji kuboreshewa zaidi eneo hilo. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Hata hivyo, wakati Simba inafanikisha uhamisho wa mshambuliaji huyo anayetazamiwa kuongeza nguvu eneo hilo, inaelezwa kuwa, haikuwa rahisi kumnasa kutokana na ugumu kiasi cha kocha na skauti wa timu hiyo kuumiza kichwa.

Inaelezwa kwamba Klabu ya Simba imetumia kiasi cha dola za Kimarekani 250000 sawa na Milioni 677 za Kitanzania, na huo unakuwa usajili mkubwa zaidi kwa klabu ya Simba msimu huu wa 2024/25.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Ateba Leonel Christian kama anavyofahamika huko nchini kwao Cameroon, akiwa USM Alger hakuwa na namba nzuri sana kutokana na kubadilishiwa majukumu yake.

Kiasili Ateba ni mshambuliaji wa kati na muda wote huwa anacheza kama namba 9, lakini baada ya kufika Algeria kocha wa USM Alger alianza kumchezesha winga hii ikamfanya kuwa na asisti nyingi kuliko magoli.

Ujio wake utaenda kumpa msaada Steve Mukwala ambaye amekuwa akiteseka kwenye umaliziaji licha ya kuwa na mikimbio mizuri na kuwasumbua mabeki wa timu pinzani.

Ateba amechukua nafasi ya Kipa wa klabu ya Simba Ayoub Lakred ambaye, alipata majeraha yatakayomfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu kidogo.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe