SIMBA YASHUSHA STRAIKA KUTOKA CAMEROON

UONGOZI wa Simba umebainisha kwamba upo kwenye mpango wa kukamilisha usajili wa mshambuliaji ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Ipo wazi kwamba Simba ni namba tatu kwenye Ngao ya Jamii 2024/25 imeshuhudia safu ya ushambuliaji ikifunga bao moja pekee na mtupiaji ni kiungo Saleh Karabaki ilikuwa dakika ya 10 kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Coastal Union ya Tanga.SIMBASafu ya ulinzi inayoongozwa na Che Malone ni bao moja ilifungwa katika nusu fainali ya pili dhidi ya Yanga dakika ya 44 na mtupiaji alikuwa ni Maxi Nzengeli dakika ya 44 kwa pasi ya Prince Dube huku mshambuliaji wa Simba, Joshua Mutale akikwama kufunga kwenye mechi hizo mbili.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa kuna maboresho ambayo yanafanyika ndani ya Simba hasa kwenye eneo la ushambuliaji kwa kuwa hapo bado hawajawa imara zaidi.

“Tuna kikosi imara na wachezaji wenye ubora ndani ya timu na sehemu pekee ambayo tunakwenda kuifanyia maboresho zaidi ni eneo la ushambuliaji ambapo hapo bado hatujawa imara zaidi. Furaha inakuja zaidi kwa Wanasimba tutafurahi zaidi na zaidi viongozi wanafanyia kazi suala hilo.”

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kutambulishwa na Simba ni Lionel Ateba raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25 ambaye aliwahi kucheza Klabu ya USM Alger.

Acha ujumbe