Simba Mshindi wa Ttau Ngao

Klabu ya Simba imefanikiwa kupata ushindi wa goli moja kwa bila katika mchezo wa mshindi wa tatu Ngao ya hisani kati yao na klabu ya Coastal Union kutoka jijini Tanga.

Ni Salehe Karabaka ambaye aliwapa uongozi klabu ya Simba mapema dakika ya 11 kwa kufunga bao pekee ambalo limewapa wekundu wa msimbazi ushindi,Goli hilo limetokana na Simba kuliandama lango la Coastal mara kwa mara mwanzoni mwa mchezo mpaka kufanikiwa kupata goli hilo.simbaWekundu wa msimbazi walionekana kutengeneza nafasi mara kadhaa haswa kipindi cha kwanza lakini hawakufanikiwa kutumia nafasi nyingi walizozitengeneza, Hii inatokana na kusuasua kwa safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo jambo ambalo kocha Fadlu Davids ameshalieleza siku kadhaa nyuma.

 Licha ya kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Coastal Union bado klabu ya Simba inaonekana kutokaa sawa, Huku kiwango cha mchezo wa leo kikiwa kimeshuka kulinganisha na kiwango walichokionesha dhidi ya watani zao Alhamisi ya wiki hii.

 

 

Acha ujumbe