Arteta: Nketiah Anaweza Kusalia Arsenal

Baada ya mshambuliaji wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Uingereza Eddie Nketiah kuripotiwa atatimka klabuni hapo kuelekea klabu ya Olympique Marseille kocha Mikel Arteta ameweka wazi kuna asilimia za kusalia ndani ya timu hiyo.

Kocha Mikel Arteta ameulizwa kuhusiana na mustakabali wa Nketiah kusalia ndani ya Arsenal na kocha huyo ameweka wazi kua wachezaji wengi waliopo ndani ya klabu hiyo kwasasa wana asilimia kubwa wanaweza kusalia ndani ya timu hiyo, Hii inatoa taswira pia kua kuna uwezekano mchezjai huyo akasalia ndani ya viunga vya Emirates.artetaKumekua na ripoti kadhaa kua mshambuliaji Nketiah amekubaliana maslahi binafsi na klabu ya Olympique Marseille ya kule nchini Ufaransa, Lakini kutokana na kauli ya kocha wa Arsenal aliyoitoa leo ni wazi kua kuna uwezekano mshmbuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza akasalia ndani ya viunga vya Emirates.

Klabu ya Arsenal wanahusishwa na washambuliaji kadhaa sokoni lakini hakuna ofa ambazo zimepelekwa kawa vilabu husika jambo ambalo linaonesha huenda kikosi cha kocha Arteta kisiongeze mshambuliaji, Hivo Nketiah anaweza akasalia ndani ya kikosi hicho kuelekea msimu wa 2024/25.

Acha ujumbe