Arteta Amkaribisha Calafiori kwa Furaha Klabuni

Kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta ameelezea furaha yake kuhusu matarajio ya kufanya kazi na mchezaji wa kimataifa wa Italia Riccardo Calafiori, ambaye jana amekamilisha rasmi uhamisho wake wa kwenda London Kaskazini kwa mkataba wa kudumu kutoka Bologna.

Arteta Amkaribisha Calafiori kwa Furaha Klabuni

Arteta alisema kuwa Calafiori ni mtu na mchezaji mkubwa ambaye ana ujuzi maalum ambao utawasaidia The Gunners kuimarika katika harakati zao za kunyanyua taji kubwa.

Kocha huyo aliongeza kuwa anatazamia kufanya kazi na beki huyo wa zamani wa Basel na Roma kwa miaka mingi ijayo.

“Tunamkaribisha Riccardo na familia yake Arsenal. Ni usajili mzuri na anatupa nguvu kubwa ya kuimarisha ulinzi wetu,” Arteta alisema katika taarifa kwenye tovuti ya klabu.

Arteta Amkaribisha Calafiori kwa Furaha Klabuni

Riccardo ni haiba kubwa na ana ujuzi maalum ambao utawafanya kuwa na nguvu wanaposukuma kushinda mataji makubwa. Tayari ameonyesha maendeleo makubwa katika misimu ya hivi karibuni na maonyesho yake kwa Bologna na Italia, na maendeleo yake katika mwaka uliopita yakiwa ya kuvutia sana.

“Tunatazamia kufanya kazi na Riccardo, kumuunganisha kwenye kikosi, na kumuunga mkono katika miaka ijayo.”

Calafiori anajiunga na Arsenal kwa bei iliyoripotiwa ya chini ya €50m huku takriban €5m katika bonasi zikijumuishwa katika ada hiyo. Mchezaji huyo, ametia saini kandarasi ya miaka mitano Emirates na anadaiwa mshahara wa €4m kwa msimu.

Arteta Amkaribisha Calafiori kwa Furaha Klabuni

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliwasili nchini Uingereza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya Jumamosi asubuhi, na tangu wakati huo amesafiri kwenda Marekani kukutana na kocha wake mpya na wachezaji wenzake katika kambi yao ya maandalizi ya msimu mpya.

Acha ujumbe