Mourinho Akanusha Tetesi za Kujiunga na Real Madrid

Kocha wa Benfica, Jose Mourinho amesema hakuna mawasiliano yoyote kati yake na Real Madrid licha ya tetesi zinazoendelea kumhusisha na kurejea katika klabu hiyo ya Hispania msimu ujao.

Mourinho Akanusha Tetesi za Kujiunga na Real MadridMourinho, ambaye aliwahi kuifundisha Real Madrid kati ya mwaka 2010 hadi 2013, anatajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaoweza kuchukua nafasi ya kocha wa sasa Alvaro Arbeloa ambaye yuko hatarini kuondolewa baada ya timu hiyo kushindwa kutwaa taji kubwa kwa msimu wa pili mfululizo. “Hakuna mtu yeyote kutoka Real Madrid ambaye amewahi kuzungumza nami. Naweza kuthibitisha hilo,” alisema Mourinho.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa aliongeza kuwa amezoea kusikia taarifa za aina hiyo kutokana na muda mrefu aliokaa kwenye soka la kimataifa. “Nimekuwa kwenye mpira kwa miaka mingi sana, na nimezoea mambo kama haya… lakini hakuna chochote kutoka Real Madrid,” alisisitiza.

Mourinho Akanusha Tetesi za Kujiunga na Real MadridWakati huo huo, Rais wa Real Madrid Florentino Perez alimchagua Arbeloa kuchukua nafasi ya Xabi Alonso mwezi Januari, lakini matokeo hayajawa ya kuridhisha huku timu hiyo ikiwa nyuma kwa pointi 11 dhidi ya vinara Barcelona kwenye msimamo wa La Liga.

Mourinho Akanusha Tetesi za Kujiunga na Real MadridReal Madrid pia walitolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Bayern Munich, jambo lililoongeza presha kwa benchi la ufundi.

Mourinho Akanusha Tetesi za Kujiunga na Real MadridMourinho, ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja uliobaki na Benfica, alisema anaendelea kujikita na majukumu yake ya sasa licha ya tetesi hizo. “Nina mwaka mmoja uliobaki kwenye mkataba wangu na Benfica, na hicho ndicho kilicho muhimu kwa sasa,” alihitimisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.