Nyota wa zamani wa Tottenham Hotspur, Erik Lamela, amezungumzia hali yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyonga kufuatia kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 33. Lamela alilazimika kutundika daruga baada ya kusumbuliwa na maumivu ya muda mrefu yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 11.
Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii baada ya upasuaji huo, Lamela alionesha matumaini mapya ya kuanza maisha bila maumivu. “Nina maumivu kidogo, lakini kwa nyonga yangu mpya natumaini kifaa hiki bandia kitakuwa mwanzo wa maisha bila maumivu,” alisema, huku akiwashukuru mashabiki waliompa sapoti.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika mahojiano na TyC Sports, nyota huyo wa zamani wa Argentina alieleza kuwa alifikia uamuzi wa kustaafu kutokana na hali yake ya kiafya. “Nilistaafu kutokana na tatizo la kimwili lililokuwa likinisumbua kwa muda mrefu. Nilitaka kumaliza kazi yangu kwa njia bora zaidi nikifurahia kadri nilivyoweza licha ya changamoto,” alifafanua.
Lamela alibainisha kuwa hali yake ilichangiwa na kuchakaa kwa gegedu pamoja na kusumbuliwa na osteoarthritis iliyofikia hatua ya juu. “Miaka ya mwisho ilikuwa migumu zaidi kwa sababu sikuweza tena kufanya mazoezi kama zamani. Nyonga yangu haikuweza kuhimili kiwango cha juu cha ushindani,” aliongeza.
Akiwa ameanza soka lake katika River Plate kabla ya kupitia AS Roma na baadaye kung’ara Spurs, Lamela alijijengea jina kubwa kwa staili yake ya kipekee, hasa mabao ya kuvutia kama yale ya “rabona” yaliyowavutia mashabiki wengi.
Baada ya kuondoka England, aliendelea na maisha ya soka katika Sevilla FC na baadaye AEK Athens ambako alimalizia taaluma yake. Kwa sasa, Lamela amerejea Sevilla akihudumu katika benchi la ufundi, akianza ukurasa mpya wa maisha yake ndani ya mchezo huo.

