Kocha wa Spurs Roberto De Zerbi wa amesema anataka kuondoa kabisa mawazo hasi ndani ya kikosi chake wakati timu hiyo ikiendelea kupambana kujinusuru kushuka daraja katika Premier League. Spurs kwa sasa wako pointi mbili nyuma ya eneo salama huku zikiwa zimebaki mechi nne kabla ya msimu kumalizika.
Spurs walipata ushindi wao wa kwanza wa ligi tangu Desemba baada ya kuifunga Wolverhampton Wanderers mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini walipata pigo kubwa kufuatia kiungo mshambuliaji Xavi Simons kupata jeraha baya la goti ambalo limemaliza msimu wake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza kabla ya mchezo dhidi ya Aston Villa, De Zerbi alisisitiza umuhimu wa kuondoa fikra hasi ndani ya timu.
“Nataka kuwa wazi kabisa. Changamoto kubwa sasa ni kunyamazisha sauti ya ndani yetu kwa wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki,” alisema.
Aliongeza kuwa mawazo hasi yamekuwa yakitoa visingizio visivyo na msingi ndani ya kikosi. “Sauti hii inazalisha mawazo kama hatuna bahati, tuna majeraha mengi, tumempoteza Simons, madaktari si wazuri au hata uwanja si mzuri. Haya yote ni mambo hasi na hayana ukweli,” alisisitiza kocha huyo raia wa Italia.
Kocha huyo aliweka wazi kuwa Spurs wana uwezo wa kushindana na timu yoyote licha ya hali yao ya sasa. “Tunakwenda kucheza na moja ya timu bora, lakini tukishinda Villa Park si muujiza. Tuna ubora wa kufanya hivyo, tunahitaji tu kuwa na mtazamo chanya,” alisema.
Kuhusu hali ya kiungo James Maddison, De Zerbi alisema mchezaji huyo anaweza kuwa msaada mkubwa katika mechi zilizobaki.
“Ningependa kumtumia kwa sababu ni mchezaji wa kipekee, lakini lazima tuangalie utimamu wake wa mwili. Naam, anaweza kuwa muhimu katika mechi chache zijazo,” aliongeza.
Aidha, De Zerbi aliahidi kuwa klabu hiyo itafanya maboresho makubwa katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi ili kuepuka changamoto kama hizi msimu ujao.
“Katika majira ya kiangazi tunaweza kufanya kila kitu tutajadili mpira, usajili na maboresho yote tunayohitaji. Tutafanya hivyo,” alihitimisha.

