JKT Waongeza Viti 2000 Uwanja wa Meja Gen. Isamuhyo Kuelekea Kariakoo Derby

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linaendelea na maboresho ya Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ikiwa ni maandalizi ya derby kubwa ya Kariakoo kati ya Simba SC na Yanga SC inayotarajiwa kuchezwa Jumapili.

JKT Waongeza Viti 2000 Uwanja wa Meja Gen. Isamuhyo Kuelekea Kariakoo DerbyMaboresho hayo yanalenga kuhakikisha uwanja unakuwa tayari kupokea idadi kubwa ya mashabiki wanaotarajiwa kujitokeza. Katika hatua hiyo, JKT imeanza ujenzi wa majukwaa mapya ya muda kwa lengo la kuongeza viti 2,000 kabla ya mchezo huo. Ongezeko hilo litaufanya uwanja huo kufikia uwezo wa kuchukua mashabiki 10,000 kutoka 8,000 waliokuwepo awali.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumzia maboresho hayo, chanzo kutoka JKT kilibainisha kuwa lengo ni kupunguza changamoto ya uhaba wa nafasi. “Tunafanya kila juhudi kuhakikisha mashabiki wengi zaidi wanapata nafasi ya kushuhudia dabi hii muhimu,” kilieleza chanzo hicho.

JKT Waongeza Viti 2000 Uwanja wa Meja Gen. Isamuhyo Kuelekea Kariakoo DerbyAwali, uwanja huo uliokuwa ukitumiwa na Simba kwa michezo yake ya nyumbani ulikuwa na uwezo mdogo, jambo lililosababisha baadhi ya mashabiki kuwa na hofu ya kukosa nafasi katika mechi kubwa kama hii. Maboresho haya yanatarajiwa kupunguza changamoto hiyo, ingawa si kwa kiwango kikubwa sana.

JKT Waongeza Viti 2000 Uwanja wa Meja Gen. Isamuhyo Kuelekea Kariakoo DerbyDabi ya Kariakoo imekuwa ikivuta hisia za mashabiki wengi kutokana na ushindani mkubwa kati ya timu hizo kongwe za Tanzania. “Ni mchezo ambao kila mmoja anataka kushuhudia, hivyo maandalizi haya ni muhimu sana,”

JKT Waongeza Viti 2000 Uwanja wa Meja Gen. Isamuhyo Kuelekea Kariakoo DerbyKwa mujibu wa taarifa rasmi, viingilio vya mchezo huo vimetangazwa kuwa ni Sh15,000 kwa kawaida, VIP B Sh30,000 na VIP A Sh50,000. Matarajio ni kuwa uwanja huo utajaa mashabiki watakaokwenda kushuhudia pambano hilo kubwa la watani wa jadi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.