Kuelekea dabi ya Kariakoo itakayopigwa Jumapili saa 12:00 jioni kwenye dimba la Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam, makocha wa Simba SC na Yanga SC wameweka wazi mikakati na presha ya mchezo huo mkubwa. Simba wakiwa wenyeji wanahitaji ushindi ili kuendelea kubaki kwenye mbio za ubingwa huku Yanga wakisaka kulipiza kisasi cha kipigo cha hivi karibuni.
Kocha mkuu wa Simba, Steve Barker, amesisitiza umuhimu wa timu yake kuwa na ubora na mapambano ya hali ya juu ndani ya uwanja. “Tunahitajika tuwe bora zaidi uwanjani kuliko wao, tunatakiwa kuwa na nguvu na upambanaji muda wote, tukifanya hivyo tutaishika mechi,” alisema Barker akionyesha kujiamini kuelekea pambano hilo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Barker aliweka wazi uzito wa mchezo huo katika mbio za ubingwa, akionya kuwa matokeo mabaya yanaweza kuimaliza Simba. “Kama tutapoteza kesho tutakuwa tumejitoa kwenye mbio za ubingwa maana sioni Yanga wakiangusha alama huko mbeleni,” aliongeza kocha huyo, akionesha namna mchezo huo ulivyo na presha kubwa kwa upande wao.
Kwa upande wa Yanga, kocha wao Pedro Goncalves amesema wamejiandaa vizuri kiufundi na kiakili kuhakikisha wanapata ushindi. “Ni mchezo mwingine ambao una mahitaji makubwa na tofauti, naamini tutakuwa na kiwango kizuri kesho dhidi ya Simba, tumefanyia kazi kila kitu kuhakikisha tunashinda na kiakili tupo vizuri,” alisema Pedro Goncalves
Yanga wanaingia kwenye dabi hiyo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza kwa Simba siku chache zilizopita katika Kombe la Muungano lililochezwa Zanzibar, ambapo walikubali kichapo cha bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Selemani Mwalimu, na kuifanya Simba kutwaa ubingwa huo. Matokeo hayo yanaongeza ushindani na presha kwa Yanga wanaotafuta kulipiza kisasi mbele ya mashabiki wa watani wao.

