Barcelona Wanataka Kumuuza De Jong

Klabu ya Barcelona inaelezwa ipo tayari kumuuza kiungo wake raia wa kimataifa wa Uholanzi Frenkie De Jong katika dirisha hili kubwa la majira ya kiangazi.

Barcelona wako tayari kumuachia De Jong na klabu ambayo wameipa ofa ya kumnunua ni Manchester United ambayo ilikua inamfatilia kiungo huyo kwa muda mrefu, Miamba hiyo ya soka kutoka nchini Hispania inatambua fika kua Man United kwasasa wanahaha sokoni kutafuta kiungo.barcelonaManchester United ilikua inamfuatilia Frenkie De Jong kwa miaka miwili mfululizo ambapo hawakufanikiwa kupata saini ya nyota huyo, Lakini Barca kwasasa wanaelezwa kua wako tayari kumuachia kutokana na hali ya kiuchumi ambayo inawakabili kw akipindi hichi.

Manchester United wanatafuta kiungo kwenye dirisha hili kwasasa baada ya kufanikiwa kusajili mabeki watatu na mshambuliaji mmoja, Hivo kwasasa wanahitaji kiungo ambapo Barcelona wakiwa wanahitaji kupunguza wachezaji wanaopokea mishahara mikubwa klabuni hapo wamewapa ofa Man United ya kumchukua kiungo huyo.

Acha ujumbe