Barcelona Watuma Ofa ya Pili Leipzig

Klabu ya Barcelona imetuma ofa ya pili kwa klabu ya Rb Leipzig kwajili ya kupata saini ya kiungo wa kimataifa wa Hispania klabuni hapo Dani Olmo ambapo ofa ya kwanza ilipigwa chini.

Barcelona inaelezwa kumalizana na kiungo Dani Olmo kwenye suala zima la maslahi binafsi huku sasa wanapambana kuhakikisha wanamalizana na klabu ya Rb Leipzig kwa kutoa kiasi ambacho klabu hiyo kutoka nchini Ujerumani itaridhishwa nacho ili iweze kumuachia Dani Olmo.barcelonaDani Olmo amekua mchezaji anayefuatiliwa kwa karibu kwasasa sokoni kutokana na ubora ambao ameuonesha kwenye michuano ya Euro mwaka 2024 iliyopigwa nchini Ujerumani, Manchester City nao wakitajwa kama klabu ambayo inafukzuia saini ya mfungaji bora wa Euro 2024.

Kiungo Dani Olmo inaelezwa kwa upande wake amechagua kucheza klabu ya Barcelona msimu ujao ambapo ameshakubaliana nao kila kitu, Jambo ambalo linawapa urahisi klabu hiyo kutoka Catalunya kupata saini ya kiungo huyo kwakua mchezaji mwenyewe anatamani kuitumikia klabu yake hiyo ya zamani.

Acha ujumbe