Barcelona Yahamia kwa Olmo

Klabu ya Barcelona sasa imehamia kwa kiungo wa kimataifa wa Hispania ambaye anakipiga klabu ya Rb Leipzig kutoka nchini Ujerumani anayejulikana kama Dani Olmo.

Barcelona kwasasa wamefikia katika hatua nzuri za kumpata winga wa klabu ya Athletic Club Nico Williams ambapo mazungumzo baina ya vilabu vyote yako vizuri, Hivo wameona ni wakati sasa wa kutafuta sajili nyingine kwajili ya kukiimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao na mchezaji wanaemmendeea kwasasa ni Dani Olmo.barcelonaKiungo huyo wa kimataifa wa Hispania ana mkataba na klabu ya Rb Leipzig lakini Barca wanaamini wanaweza kumshawishi kiungo huyo kujiunga nao kuelekea msimu wa 2024/25, Ikumbukwe kiungo Dani Olmo ni zao la klabu ya Barca ambapo alilelewa katika shule ya kukuza vipaji ya La Masia.

Klabu ya Barcelona hawatakua wenyewe katika mbio za kumuwania kiungo Dani Olmo ambaye alifanya vizuri kwenye michuano ya Euro 2024 na kumaliza kama mfungaji bora, Kwani vilabu kadhaa kama Manchester City, pamoja na Bayern Munich pia vinawinda huduma ya kiungo huyo lakini Barca wao wanaamini wana ushawishi zaidi na mchezaji anataka kujiunga na klabu yao.

Acha ujumbe